Kahama FM
Kahama FM
1 June 2026, 5:41 pm

”Kuanza kwa mradi wa Mpango Kabambe Kidigitali na kukamilika utaweza kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi, pamoja na kuendelea kupanga mji”
Imeelezwa kuwa miaka 25 ijayo, Wananchi wa Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga kuondokana na migogoro ya ardhi baada ya kukamilika kwa mradi wa mpango kabambe wa kidigitali (Master Plan) utakapokamilika.
Lengo la mpango huo unalenga kudhibiti ujenzi na makazi holela Pamoja na kupanga mji kuwa wa kisasa na kutenga maeneo mbalimbali kwa shughuli za kijamii, kiuchini na kiibada.

Akizungumza katika mafunzo na viongozi mbalimbali wa kata ya Malunga, mtaalamu Mshauri kutoka Kampuni ya Urban Solution (ICE EXPERT) Hamisi Mkoma, amesema mradi huo utakapokamilika mji utabadilika na kuwa wa kisasa Pamoja na kupunguza changamoto katika sekta ya miundombinu ya barabara na makazi, huku ardhi ikipanda thamani.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Malunga Hamed Haruna, amesema kuwa mradi huo utaweza kuwasaidia wananchi kupanda kwa thamani ya ardhi na kuwaomba wananchi waupokee mpango kabambe wa kidigitali.
Baadhi wa wananchi wa kata ya Malunga wakizungumza kwa nyakati tofauti akiwemo Michael Msano na Marco Makune, wamesema kuwa mpango huo utakapokamilika utasaidia kuondokana migogoro ya ardhi, pamoja na mji kupangika na kuwa salama

Mradi huo unakwenda kutekelezwa katika kata 20 za Manispaa ya Kahama, ikiwemo kata ya Kinaga, Isagehe, Mondo, Ngongwa, Nyandekwa, Kilago na Wendele zinazo kwenda kubadilika kutoka vijiji na vitongoji na kuwa mitaa.