Kahama FM

Wananchi Kahama watakiwa kuwa waaminifu katika shughuli zao za kiuchumi

7 May 2026, 5:24 pm

Askofu wa jimbo katoliki la Kahama Christopher Ndizeye( Picha na Sebastian Mnakaya)

Wananchi wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuendelea kuwa waaminifu na waadili katika shuguliza zao mbalimbali za kijamii na kiuchumi pasipo kujitafutia faida kubwa.

Na Mwandishi wetu

Wito huo umetolewa na Askofu wa jimbo katoliki la Kahama Christopher Ndizeye, wakati wa kufunguliwa kwa tawi la benki ya biashara ya Mkombozi wilayani Kahama mkoani Shinyanga, ambapo amesema kuwa ili tuwe waaminifu tunapaswa kufanyakazi halali itakayompendeza Mungu.

Sauti ya Askofu wa jimbo katoliki la Kahama Christopher Ndizeye

 Kwa upande wake, Mkurugenzi wa benki ya Mkombozi Respige Kimati, amesema kuwa kufunguliwa kwa benki hiyo ni Suluhu kwa Wafanyabiashara wadogo hususani Wajasiriamali wadogo ambao waliokuwa wakikabiliwa na tatizo la Mikopo umiza baada ya taasisi hiyo kuanzisha mfumo maalum wa kutoa mikopo ili kuwakwamua kiuchumi.

Sauti ya Mkurugenzi wa benki ya Mkombozi Respige Kimati

Nae, baadhi ya wafanyabiashara wilayani Kahama akiwemo Specioza Mahendeka na Ezekia Mafuru wamesema kuwa kupitia benki hiyo hawatakopa mikopo yenye riba nafuu, huku wakiachana na mikopo umiza na yenye riba kubwa.

Sauti za wafanyabiashara wa wilaya ya Kahama Specioza Mahendeka na Ezekia Mafuru