Kahama FM
Kahama FM
17 July 2026, 4:45 pm

‘‘Kwa sasa serikali imechukua mkandalasi mpya mwenye uwezo wa kukamilisha mradi huo kwa wakati’’
Mbunge wa jimbo la Kahama Mjini mkoani Shinyanga Benjamini Ngayiwa, amewahidi wananchi wa Manispaa Kahama ya kuwa ifikapo January 2027 ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami ya mjini kati utakamilika, huku ukigarimu kiasi shilingi bilion 25.
Nyayiwa amesema hayo, wakati wa hafla ya michezo ya kitamaduni iliyofanyika katika ukumbi wa Miligo Hall katika Manispaa ya Kahama, ambapo amesema kuwa barabara hiyo imechelewa kutokana na mkandalasi wa kwanza kushindwa kukamili ujenzi kwa wakati, hali iyosababisha kuvunja kwa mkataba na kumpatia mkandalasi mpya.

Mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanue Cherehan amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo na kahama utakuwa mji wa kisasa, huku Ngayiwa akisema kuwa serikali imekuwa ikiendelea kutekeleza miradi mingine mikubwa ikiwemo ujenzi wa stendi ya kisasa na masoko kwa mradi wa benki ya dunia (TACTIC).

Kwa upande wake, mwenyekiti wa chama cha madereva na wamiliki wa pikipiki za biashara mkoa wa Shinyanga Iddsam Mapande amesema kuwa kukamilika kwa barabara hizo zitaondoa adha wanazokutanazo madereva kwa ubaovu wa barabara hizo.

Nao, baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Kahama wakizungumza kwa nyakati tofauti, akiwemo John German na Fadhili Kipindula, wameishuru serikali kwa kuanza kwa ujenzi huo uliyosimama kwa muda mrefu na kuomba ukamilike kwa wakati ili wananchi kuondoka na adha wanazokuta nazo kwa kipindi hiki.
Ikumbukwe, Kampuni ya SICHUAN ROAD & BRIDGE CO.LTD kusitishiwa mkataba wa ujenzi barabara baada ya kukiuka masharti ya kimkataba na kupewa kampuni nyingine ya china Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) ambo sasa wanakamilisha mradi huo na ukitakiwa kukamilika ndani ya miezi 8.