Kahama FM

Manispaa ya Kahama yatia saini ya ujenzi wa wa barabara ya lami

28 May 2026, 1:32 pm

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Prof. Riziki Shemdoe, ameshuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa barabara katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga kupitia Mradi wa TACTIC.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika eneo la Phantom, Kata ya Nyasubi wilayani Kahama, Prof. Shemdoe ameutaka mkandarasi wa mradi huo, kampuni ya China ya Civil Engineering Construction Corporation (CCECC), kuhakikisha unakamilika kwa wakati ili kuwaondolea wananchi adha na changamoto zinazotokana na ubovu wa miundombinu ya barabara.

Sauti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Prof. Riziki Shemdoe

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita amesema serikali ya mkoa huo haitakuwa tayari kuona wananchi wakikumbwa na changamoto zinazokwaza maendeleo, hali ambayo ni kinyume na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita

Naye Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, Benjamin Ngayiwa ameipongeza serikali kwa hatua hiyo ambayo imekuwa ni matarajio ya wananchi wa Kahama kwa muda mrefu, huku akiomba mkandarasi huyo kuongezewa kipande cha barabara cha kilomita moja eneo la Malunga (Mashine za Mpunga).

Sauti yaMbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, Benjamin Ngayiwa

Kwa upande wake, Mratibu wa Miradi inayotekelezwa nchini kwa ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na TAMISEMI, Mhandisi Humphrey Kanyenye, amesema mradi huo utagharimu shilingi bilioni 25 na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi nane.

Sauti ya Mratibu wa Miradi inayotekelezwa nchini kwa ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na TAMISEMI, Mhandisi Humphrey Kanyenye