Kahama FM

TAKUKURU Kahama yapongezwa

4 June 2026, 2:16 pm

Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda akizungumza katika mafunzo (Picha na Sebastian Mnakaya)

Serikali wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeipongeza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), kwa juhudi za mapambano ya kuzia rushwa katika wilaya hiyo yenye halmashauri tatu.

Na mwandishi wetu

Hayo yamesemwe na Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda wakati akifungua semina ya walimu walezi wa klabu za kupinga rushwa katika shule za sekondari kutoka manispaa ya Kahama,halmashauri ya Ushetu na halmashauri ya msalala.

Nkinda amesema kuwa TAKUKURU Wilayani Kahama wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzuia na kupambana na rushwa na kwamba wilaya ya Kahama kesi za rushwa zimepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na juhudi za takukuru ikiwemo kutoa elimu kwa jamii.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Kahama Abdallah Urari amesema kuwa wamefungua klabu za wapinga rushwa katika vyuo vyote Kahama na shule za sekondari na kwamba wataendelea kufungua klabu hizo katika shule zote za msingi wilaya ya Kahama.

Sauti ya Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Kahama Abdallah Urari

Kwa upande wao baaadhi ya walimu walezi Lubango Joseph kutoka shule ya sekondari kishimba na Fatuma kidubo kutoka shule ya sekondari Nyahanga wamesema kuwa wamefurahi kupata mafunzo hayo kwani walikuwa wanaendesha klabu hizo bila mafunzo yoyote na kwamba klabu hizo zitawasaidia wanafunzi kujua madhara ya rushwa na kuwa mabalozi katika jamii.

Sauti za walimu walezi Lubango Joseph kutoka shule ya sekondari kishimba na Fatuma kidubo kutoka shule ya sekondari Nyahanga