Kahama FM

TRA Kahama, yatoa msaada kwa watoto wanaoishi mazingira magumu

25 June 2026, 6:25 pm

Akikabidhi msaada huo, Meneja wa TRA Mkoa wa kikodi Kahama, Wisaka Kamwamu (Picha na Sebastian Mnakaya)

”Tunapaswa kuisaidia jamii hii ambayo inaishi katika mazingira maguru kwa chochote ulichojaaliwa na Mwenyezi Mungu”

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi Kahama imetoa msaada wa mahitaji mbalimbali katika Kituo cha Kulelea Watoto wanaotokana na Mazingira Magumu cha Mvuma, kilichopo Kata ya Nyasubi, kuelekea maadhimisho ya miaka 30 ya kuanzishwa kwa TRA tangu mwaka 1995.

Akikabidhi msaada huo, Meneja wa TRA Mkoa wa kikodi Kahama, Wisaka Kamwamu, amesema mamlaka hiyo imeamua kurejesha shukrani kwa jamii kwa kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum na kusisitiza umuhimu wa wananchi kulipa kodi kwa hiari kwa kuwa ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa.

Sauti ya Meneja wa TRA Mkoa wa kikodi Kahama Wisaka Kamwamu

Kwa upande wake Mkaguzi wa Kodi, Estar Malya, amesisitiza umuhimu wa TRA kushirikiana na jamii, huku akieleza kuwa matumizi ya teknolojia yamerahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali za kodi kwa wananchi bila usumbufu.

Sauti ya Mkaguzi wa Kodi Kahama Estar Malya

Kwa upande wake, Msimamizi wa Kituo cha Mvuma, Everist Magambo, ameishukuru TRA kwa msaada huo na kueleza kuwa kituo hicho kinakabiliwa na changamoto za ukosefu wa bima ya afya kwa watoto, nishati mbadala na vifaa vya michezo.

Sauti ya Msimamizi wa Kituo cha Mvuma, Everist Magambo

Mahitaji yaliyotolewa ni pamoja na mchele, unga, mafuta ya kupikia, sukari na madaftar, ambapo kwa sasa Kituo hicho kwa sasa kinahudumia watoto 50, wakiwemo mabinti 30 na wavulana 20.