Kahama FM

Wadau wachangia zaidi ya mifuko ya saluji 200 kwa ajili ya uzio wa Kahama Orphanage Center

1 June 2026, 7:04 pm

Mgeni rasmi Sultan Mitimingi akizungumza katika halfa hiyo (Sebastian Mnakaya)

Uongozi huo umeeleza kuwa licha ya mafanikio yaliyopo, kituo bado kina mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula, mavazi, vifaa vya shule na maboresho ya miundombinu, hivyo umeomba wadau wengine kuendelea kujitokeza kusaidia.

Wadau wa maendeleo wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamejitokeza wa wingi kuchangia zaidi ya mifuko ya saruji 200 na fedha kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa kituo cha kulelea watoto wanaishi katika mazingira magumu Kahama Orphanage Center ili kuboresha usalala wa watoto hao.

Akizungumza katika siku ya kusherekia miaka 12 kwa kuanzishwa kituo hicho, mgeni rasmi Sultan Mitimingi amesema kuwa ni ibada kwa watu kujitoa na kuwasaidia watoto hao, huku jamii ikihaswa kushirikiana katika kuwalea na kuwahudumia watoto wenye uhitaji maalumu katika kituo hicho

Sauti ya mgeni rasmi Sultan Mitimingi

Msaidizi wa Kahama Peace Orphanage Center Ustadhi Abubakar Issa

Awali, Mkurugenzi wa Msaidizi wa Kahama Peace Orphanage Center Ustadhi Abubakar Issa akisoma taarifa ya kituo hicho amesema kilianza mwaka 2014 kikiwa na watoto 7 na sasa kina jumla ya watoto 93, wavulana 50 na wachina 43, huku kikikabiliwa na changamoto ya uzio na kuomba wadau mbalimbali wa maendeleo kuwasaidia ujenzi wa uzio huo, unao gharimu kiasi cha shilingi 82,000,000.

Sauti ya Msaidizi wa Kahama Peace Orphanage Center Ustadhi Abubakar Issa

Mradi wa ujenzi wa uzio katika Kahama Orphanage Center unatarajiwa kukamilika baada ya kupatikana kwa michango hiyo, huku wadau wakiahidi kuendelea kushirikiana na kituo hicho katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto wanaolelewa hapo.