Kahama FM
Kahama FM
25 June 2026, 6:52 pm

‘‘Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) mkoani Shinyanga watakiwa kuongeza udhibiti wa makosa hayo ya jinai badala ya kutumia nguvu kubwa kupambana nayo’’
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, amewataka viongozi na watendaji mkoani humo kusimamia kwa weledi na uadilifu miradi ya maendeleo ili kuhakikisha thamani ya fedha za umma inaonekana na wananchi kupitia huduma bora na miradi yenye tija.
Akifungua warsha ya usimamizi wa miradi ya maendeleo iliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na TAKUKURU, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Aidha, Mhita ameonya dhidi ya vitendo vya rushwa, ubadhirifu wa fedha za umma na matumizi mabaya ya madaraka, akisisitiza kuwa Mkoa wa Shinyanga hautamvumilia yeyote atakayehujumu rasilimali za umma.