Kahama FM

Madiwani Kahama watakiwa kufanya mikutano mara kwa mara kwa wananchi wao

15 May 2026, 2:26 pm

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Frank Nkinda (Sebastian Mnakaya)

Serikali wilayani Kahama mkoani Shinyanga, imewataka madiwani kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo yao ili kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi, ambao wengi wao wanakosa majukwaa ya kuwasilisha matatizo yao.

Amesema uzoefu unaonesha kuwa kila anapofanya mikutano na wananchi, hupokea maoni na malalamiko mengi hali inayoashiria kuwa baadhi ya madiwani hawafanyi mikutano ya mara kwa mara katika maeneo yao.

Ameyazungumza hayo katika kikao cha Baraza la Madiwani cha Manispaa ya Kahama cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2025/2026, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, akisema mikutano hiyo ni muhimu kwa kuwawezesha wananchi kueleza kero zao pamoja na kufahamu utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda