Kahama FM
Kahama FM
8 July 2026, 12:46 pm

”Orodhesheni magari mabovu yote pamoja na gharama zake ili yatengenezwe na kuanza kufanyakazi”
Madiwani wa Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameiomba halmashauri hiyo, kuorodheshwa kwa magari mabovu na gharaza za utengenezaji ili kuweza kufanya matengenezo na kuanza kutumika.
Ombi hilo limetolewa na diwani viti malaam Ester Matona na diwani wa kata ya Kinamapula Samweli Adrian, wakati wa baraza maalum la kupitia taarifa ya mdhibiti na mkaguazi mkuu wa hesabau za serikali (CAG) katika halmashauri la Ushetu.

Diwani Ester amesema kuwa wanaungana na menejimenti kwa ushauri juu ya matengenezo ya magari hayo, huku diwani wa kata ya Kinamapula Adriani kutengenezwa kwa magari mabovu ni muhimu kwa ajili ya ufanisi wa kazi kwa watumishi.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita amesema kuwa kutenganezwa kwa magari hayo, itakwenda kusaidia na kuboresha na kuimarisha ufanisi wa kazi kwa watumishi katika kutekeleza na kuitembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali.

Kaimu afisa mipango wa halmashauri ya Ushetu Charles Machuba, akiwasilisha taarifa ya hoja za CAG, majibu ya menejimenti na hali utekelezaji wa mapendekezo ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2025/2026, amesema kuwa menejimenti inapaswa kuchukua hatua ya kutenga fedha kwa ajili ya matengenezo.
