Kahama FM
Kahama FM
13 August 2026, 8:01 pm

”Ni lini eneo hilo litaanza kujengwa viwanda vya uchenjuaji wa madini ya dhahabu”
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga imetanga eneo la Mwagala kata ya Kinaga kwa ajili ya kujengwa kwa viwanda vya kuchenjua madini ya dhahabu (ELUTION PLANT), inaratajiwa kuanza baada ya kukamilika kwa miundombinu muhimu, ikiwemo barabara, Umeme na Maji.
Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Masud Kibeti, katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya nne ya mwaka 2025/2026, wakati akijibu swali la diwani wa kata ya Majengo Zacharia Soko aliyetaka kujua ni lini eneo hilo litanzaa kujengwa viwanda hivyo.

Aidha, Kibetu amesema kuwa serikali itaanza kutekeleza hilo baada ya kuweka miundombinu muhimu ili viwanda hivyo viweze kujengwa, huku akisema kuwa kwa mwaka wa fedha 2026/2027 utaanza kutekelezwa.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Majengo Zacharia Soko amesema kuwa tangu kutengwa kwa eneo hilo mpaka sasa hakuna kinachoendelea na kuomba kujua lini utaanza kujengwa kwa viwanda hivyo vya uchenjuaji wa madini ya dhahabu.
