Kahama FM
Kahama FM
22 August 2026, 8:12 pm

Waraibu wa matumizi ya dawa za kulevya wanaopatiwa matibabu katika Jengo la Waraibu lililopo Hospitali ya Manispaa ya Kahama mkaoni Shinyanga, wameiomba Serikali kuongeza juhudi za kupambana na wauzaji na wasambazaji wa dawa hizo.
Ombi hilo wamelitoa wakati Mwenge wa Uhuru ukizidua jengo hilo jipya lililojengwa kwa ajiri ya malezi ya waraibu, lenye thamani ya zaidi ya shilingi Milion 400 lililoanza kutoa huduma mwezi wa Mei mwaka huu, na Linalenga kuwapatia matibabu, malezi na ushauri waraibu ili waweze kurejea katika Hali yao kawaida.

Baadhi ya warahibu wanaotoka maeneo mbalimbali wilayani humo, akiwemo Mutazi Maganga na Asia Wanga ameomba serikali kutilia mkazo la kuendelea kudhibiti madaya ya kulevya ili vijana waendeleo kuwa salama kwa kutopatikana kwa madawa hayo.
Akizungumza baada ya uzinduzi na kupokea maombi ya waraibu, Mkimbiza Mwenge Kitaifa, Wazo Mang’onda, amesema kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)na Jeshi la Polisi watahakikisha wanaongeza juhudi za kukabiliana na changamoto hiyo.
Kwa upande wake Dkt, Grace Nzangamba, Msimamizi wa Waraibu Manispaa ya Kahama amesema mpaka sasa kituo kina waraibu 35 wanaopatiwa matibabu, huku kiisisitiza jamii kutosita kuwapeleka kituoni watu wenye changamoto hizo ili wapatiwe matibabu mapema kabla hali haijazidi kuwa mbaya.
Hata hivyo, Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 Unaujumbe Usemao “Tanzania yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo”.
