Kahama FM

Rc Mboni, atoa tahadhari kufuatia mvua za El Nino

1 October 2026, 1:23 am

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akikagua ujenzi wa barabara katika kata ya Jana katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama (Picha na Sebastian Mnakaya)

‘‘Tahadhari ni muhimu kabla ya kutokea kwa madhara, hivyo  wananchi na viongozi wanapaswa kuzingatia ushauri unaotolewa na watendaji wa Serikali’’

Serikali mkoani Shinyanga imewataka viongozi na watendaji wa maeneo mbalimbali kuhakikisha fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo zinatumika katika maeneo yaliyokusudiwa, huku ikisisitiza umuhimu wa kufuatilia ubora wa miradi hiyo.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo, katika kata ya Mwanase na Jana wilayani Kahama, mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, amesema kazi ya wawakilishi wa wananchi ni kuhakikisha changamoto zinazowasilishwa zinapatiwa ufumbuzi, na fedha za miradi zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Aidha, amesisitiza kuwa pamoja na kuangalia matumizi ya fedha za miradi, Serikali itaendelea kufuatilia ubora wa barabara na miundombinu mingine, kutokana na tahadhari iliyotolewa kuhusu uwezekano wa mvua za vuli kunyesha kwa kiwango cha juu kuliko wastani.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita

Nae, Mhandisi wa halmashauri ya Msalala, akisoma taarifa ya mradi wa barabara inayotekelezwa na halmashauri hiyo kwa kushirikia na TARURA inaendelea kwa ajili ya mvua za EL NINO, huku baadhi ya wananchi katika halmashauri hiyo wamesema kuwa awali kabla ya ujenzi wa barabara hiyo hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba palikuwa hapapitiki.

Sauti ya Mhandisi wa Halmashauri ya Msalala na wananchi

Kwa upande wake, mbunge wa jimbo la Msalala Mabula Magangila, amesema halmashauri kwa kushirikiana na TARURA imetenga fedha kwajili ya kuzikarabati barabara kabla ya mvua kuanza kunyesha, huku diwani wa kata ya Jana Shigela Sonda amesema kilio kibukwa kwa wananchi wa maeneo hayo ni ubovu wa barabara.

Sauti ya mbunge wa jimbo la Msalala Mabula Magangila na Diwani wa kata ya Jana Shigela Sonda

Hata hivyo, endapo mvua zitaendelea kunyesha kwa kiwango kikubwa, maeneo maalumu yametengwa kwa ajili ya usalama wa wananchi yatatumika, ili kuhakikisha wananchi wanakuwa salama.