Kahama FM
Kahama FM
20 October 2026, 12:15 pm

Serikali kupitia Wizara ya Maji imeahidi kutoa Shilingi milioni 490 kwa ajili ya kukamilisha Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria katika Kata ya Isaka Jana.
Zaidi ya wakazi 2,000 wa vijiji vya Butondoro na Jana, katika Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga, wanatarajiwa kunufaika na huduma ya maji safi na salama kupitia mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria wenye gharama ya shilingi bilioni tano.
Mradi huo unalenga kuwaondolea wakazi wa maeneo hayo adha ya kutafuta maji katika visima, huku ujenzi wake ukiendelea.
Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, alipotembelea Kata ya Jana kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Butondoro, Elizabeth Bundala na Laurencia Mwandu, wanaeleza changamoto wanazokutana nazo katika upatikanaji wa maji.

Wakati huo huo, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kahama, Mhandisi Maduhu Magili, anaeleza hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo, huku Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mabula Magangila, akieleza umuhimu na manufaa yanayotarajiwa kupatikana baada ya mradi kukamilika.

Kwa upande wake, Naibu wa Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, amesema kuwa mradi huo Serikali iko katika hatua utekelezaji ili wananchi waondokane na adha ya upatikanaji wa maji.
