Kahama FM

Huduma bora za afya kwa wazee bado kitendawili-Makala

16 October 2026, 11:40 am

Katibu wa Baraza la Wazee Manispaa ya Kahama na Taifa Anderson Lymo (Picha na Sebastian Mnakaya)

Katika kipindi hiki, tunakwenda kuangazia adha wanazokutana nazo wazee wanapohitaji matibabu, ikiwemo changamoto za kiuchumi zinazoweza kuwafanya washindwe kumudu gharama za huduma za afya pamoja na mahitaji mengine muhimu wanapokuwa wagonjwa.

Hata hivyo, imenilazimu kuzungumza na Katibu wa Baraza la Wazee Manispaa ya Kahama, Anderson Lymo, ili kufahamu hali halisi ya upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wazee na changamoto wanazokutana nazo katika kupata huduma hizo.

Vilevile, nimezungumza na Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Kahama, ambaye anaeleza changamoto mbalimbali zinazowakabili wazee wanapohitaji matibabu, pamoja na namna hali zao za maisha na uwezo wa kiuchumi vinavyoathiri upatikanaji wa huduma hizo.

Je, wazee wanapata huduma za afya kwa urahisi kiasi gani? Ni adha zipi wanazokutana nazo wanapokwenda hospitalini, na ni hatua zipi zinazoweza kuchukuliwa ili kuhakikisha wanapata matibabu wanayostahili?

Sauti ya kipindi cha wazee sehemu ya pili na Sebastian Mnakaya