Kahama FM
Kahama FM
21 November 2026, 2:43 pm

‘‘Wazazi watakiwa kuwa karibu na watoto kufuatilia malezi na maendeleo yao kielimu’’
Wazazi katika Manispaa ya Kahama, wametakiwa kuongeza ushiriki wao katika malezi na elimu ya watoto kwa kuwasaidia kufanya marudio ya masomo wanayofundishwa shuleni pamoja na kutumia teknolojia kama simu na televisheni kwa namna inayochochea maendeleo yao kielimu.
Wito huo umetolewa na mgeni rasmi ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Andason Msumba Schorastica Leonard akiwa katika mahafali ya 5 Jenas and Champion English Medium Daycare ambapo, amesema pamoja na watoto kupata elimu shuleni kupitia walimu, wazazi wana wajibu wa kuwasaidia kufanya marudio ya masomo wanayofundishwa ili kuimarisha uelewa na kuongeza ufaulu.

Aidha, amewataka wazazi kutumia vizuri simu za mkononi na televisheni kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya watoto kielimu badala ya kutumia muda mwingi katika shughuli zisizo na tija.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kituo hichoJames Jallyson Lucas, ameeleza kuwa baadhi ya watoto walipoanza masomo hawakuwa na uelewa wa kutosha, lakini kupitia juhudi za walimu na usimamizi wa shule wameweza kujifunza mambo mbalimbali na kuwa tayari kwa hatua inayofuata ya elimu, huku mkurugenzi wa Glory of GodDaycare Dadsi Salum akichangia shule hiyo mikuko 5 ya saruji kwa ya uboreshaji wa miundomini ya shule hiyo.

Awali, mkuu wa shule hiyo Gadensia Willbart akisoma taarifa ya shule ameeleza kuwa watoto wenye umri wa miaka mitatu hadi mitano hujiunga na madarasa ya chekechea, ambako hufundishwa stadi mbalimbali ikiwemo kusoma na kuandika ili kuwaandaa kuanza elimu ya msingi, huku wakihakikisha watoto wanapata malezi na elimu bora itakayowasaidia kukua na msingi imara wa maisha yao ya baadaye.
