Kahama FM
Kahama FM
19 October 2026, 5:04 pm

‘‘Wapeni vipaumbele wafanyabiasha wa maeneo hayo pamoja na kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati’’
Wafanyabiashara waliopisha maeneo yao kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya Soko la Sango, Zongomela na Kituo cha Mabasi cha Nyasubi katika Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga, wametakiwa kupewa kipaumbele katika ugawaji wa vibanda baada ya miradi hiyo kukamilika.
Agizo hilo limetolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), ambapo imeutaka uongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Kahama kuhakikisha wafanyabiashara hao hawasahauliki katika utekelezaji wa miradi hiyo ya uboreshaji wa miji.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Florent Kyombo amebainisha hayo baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi ya Soko la Sango, Zongomela na Kituo cha Mabasi cha Nyasubi ambapo ameitaka Manispaa ya Kahama kuhakikisha wafanyabiashara walioathiriwa na utekelezaji wa miradi hiyo wanapewa kipaumbele katika umilikishwaji wa vibanda pindi ujenzi utakapokamilika.

Awali, Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI Hawa Subira Mwaifunga ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini, amesema kuwa baada ya miradi hiyo kukamilika bei ya kupanga vyumba vya maduka na vizimba viendane na hali ya uchumi wao, huku mhandisi mshauri mwelekezi Samwel Mtawa amesema kurugenzi wa Manispaa ya Kahama ndiye atakaye panga matumizi ya maeneo hayo.

Kwa upande wao, baadhi ya wafanyabiasha Halmashauri ya Manispaa ya Kahama akiwemo, yunge Mrtine na Mariam Masolanya wameomba kupatiwa kipaumbele kwa wafanyabiasha waliotolewa katika eneo hilo baada ya ujenzi huo kuanza.
INSERT…….WAFANYABIASHARA
