Kahama FM

Wazee Kahama hatarini kwa kutotunzwa na watoto

15 October 2026, 12:51 pm

Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Kahama John Jacob ambaye pia ni mratibu wa watu wenye ulemavu Manispaa ya Kahama (Picha na Sebastian Mnakaya)

‘‘Jamii inapaswa kuendelea kuimarisha misingi ya malezi, upendo na uwajibikaji kwa wazazi na wazee, ili kuhakikisha wanapata matunzo na huduma zinazostahili’’

Baadhi ya wazee katika Manispaa ya Kahama wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kukosa matunzo na huduma kutoka kwa watoto wao, kutokana na watoto hao kuwa na majukumu mengi ya kifamilia pamoja na changamoto za kiuchumi zinazowafanya washindwe kuwahudumia wazazi wao ipasavyo.

Akizungumzia hali hiyo, Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Kahama John Jacob amesema baadhi ya wazee wanaofika ofisini kwake wamekuwa wakieleza kushindwa kupata msaada wa kutosha kutoka kwa watoto wao, ambao nao wanakabiliwa na majukumu ya kulea watoto wao na kutafuta mahitaji ya maisha.

Aidha, amesema hali hiyo imekuwa changamoto kwa baadhi ya wazee, ambao wamejikuta wakikosa huduma muhimu kutokana na watoto wao kushindwa kumudu gharama za mahitaji yao, ikiwemo huduma za afya.

Sauti ya Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Kahama John Jacob

Kwa upande wake, Katibu wa baraza la Ushauri la Wazee Manispaa ya Kahama Anderson Lymo amesema kuwa wazee wamekuwa na hali ngumu ya kiuchumi kiasi kwamba wanashindwa kupata milo 3, huku akiwataka vijana wawahudumie wa wazee hawo bila kulazimishwa au mpaka kufikishwa katika ofisi za ustawi wa jamii.

Sauti ya Katibu wa baraza la Ushauri la Wazee Manispaa ya Kahama Anderson Lymo