Kahama FM
Kahama FM
7 July 2026, 7:02 pm

‘‘katika vitabu mbalimbali vya dini vimesisitiza juu ya watu kufanyakazi’’
Waumini wa dini ya kikristo wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameshauri kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi na kufanyakazi ili kuongeza vipato vyao na kujikwamua kiuchumi.
Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji Dkt Gwamiye wa kanisa la New Jerusalemu mpya Masaki, katika mkutano mkubwa wa injili uliyofanyika katika kata ya Nyamilango halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.
Mchungaji Dkt Gwamiye, amesema kuwa kuna baadhi wa wachungaji katika mafundisho yao wamekuwa wakiwahubilia waumini wao pokea vitu mbalimbali pasipo kufanyakazi hali inayosababisha baadhi ya kushuka kiuchumi katika maisha yao.

Aidha, Mch Dkt Gwamiye amasema kuwa hata katika vitabu mbalimbali vya dini vimesisitiza juu ya watu kufanyakazi ili waweze kutimiza majukumu yao mbalimbali ya kila siku, huku akiwataka viongozi wa dini kuhubili hivyo.

Katika hatua nyingine Mch Gwamiye, amewataka wachungaji wenzake kuwa na shughuli nyingine za kujipatia kipato tofauti na utumishi wa kuwatumikia waumini pekee.
