Kahama FM

DC Kahama atoa siku kumi na nne kwa TARURA.

September 2, 2021, 10:52 am

Serikali wilayani Kahama mkoani Shinyanga imetoa Siku 14 kwa meneja wa wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA kufanya tathmini katika barabara za mitaa zilizopo katika manspaa ya Kahama ili ziweze kufanyiwa marekebisho.

Agizo hilo limetolewa  leo na Mkuu wa wilaya ya Kahama FESTO KISWAGA katika kikao kazi cha watendaji na wenyeviti wa mitaa  pamoja na vijiji, kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Manispaa ya Kahama,lengo la kikao hicho ni kuzungumzia kero mbalimbali za wananchi ikiwemo barabara.

INSERT: KISWAGA 1

KISWAGA amesema kuna baadhi ya maeneo tayari rais SAMIA SULUHU HASSAN ametoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara lakini bado TARURA haijaanza kufanya ukarabati huo wa barabara.

INSERT:  KISWAGA 2

Katika hatua nyingine, KISWAGA amewaagiza watendaji wa kata kuwasilisha taarifa za kero mbalimbali ambazo zimejitozeka katika maeneo yao na namna ambavyo zimeweza kutatualiwa.