Kahama FM

Watatu mbaroni tuhuma za kubaka mwanafunzi

July 10, 2023, 11:58 pm

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi

Wazazi na Walezi wanatakiwa wawe karibu watoto kwa kuwalea katika maadili ya kidini,kwasababu kumekua na changamoto ya mmomonyoko wa maadili katika jamii”

Na Halima Khoya

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia vijana watatu wanaotuhumiwa kuhusika na tukio la kumbaka mwanafunzi wa shule ya sekondari Kishimba (Jina lake limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 14 akitoka dukani kwenda nyumbani.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga,ACP Janeth Magomi amesema tukio la ubakaji limetokea Julai 08 2023 majira ya saa 07 mchana kijiji cha Igumhwa kata ya Kitwana halmashauri ya wilaya Kahama mkoani humo.

Magomi amesema kuwa vijana waliokamatwa ni Dotto Venancy (18), Juma Mwita (17) na Paul Peter (17) ambao walihusika kumshambulia binti huyo aliyekuwa akitoka dukani kwenda nyumbani ambapo alibakwa na kijana aliyemfahamu kwa sura.

Amesema chanzo cha tukio hilo ni mmomonyoko wa maadili ambapo mmoja wa watuhumiwa hao ametoroka baada ya kutenda kosa hilo