Kahama FM
Kahama FM
16 June 2026, 6:00 pm

‘‘Vijana msikate tamaa wakati wa mkishughulikia kupata mikopo ya 10% inayotolewa na halmashauri, yanayotokana na mapato ya ndani’’
Vijana, wanawake na watu wenye ulemavu katika Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga wametakiwa kuacha tabia ya kukata tamaa katika ufatiliaji wa upatikanaji wa mikopo ya 10% ya halmashauri ili kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamesemwa na mkufunzi wa mafunzo ya itikadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kahama ambaye pia diwani wa kata ya Mhungula Elisha William, wakati wa kikao cha mafunzo ya itikadi aliyofanyika katika kata ya Nyahanga yakishirikisha makundi mbalimbali yakiwemo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Elisha amesema kuwa mikopo ya asilimia 10% watu wengi wanaikosa kutokana na kukosa vigenzo, huku akiwataka vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kuchamkia fursa za mikopo hiyo kwa kuzingatia masharti yaliowekwa.

Wakati huohuo, Elisha amesema kuwa lengo la Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kahama, ni kutoa mafunzo hayo, ikiwa na lengo la kuwakumbusha wanachama na vijana kufuata misingi na itikadi ya chama hicho kwa kuiishi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapindizi (CCM) kata ya Nyahanaga Lucas Matanyanga, amesema kuwa baada ya mafunzo hayo inategemea kutakuwa na mabadiliko makubwa hasa katika eneo la itikadi.
Hata hivyo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kahama kimetoa mafunzo kwa wanachama wake kwa makundi mbalimbali ili kukuwambusha na kufahamu umuhimu wa kuifuata itikadi ya chama hicho.