Kahama FM
Kahama FM
3 March 2025, 11:27 pm

Watoto wote waliofaulu kijiunga na kidato cha kwanza mkoani Shinyanga watakiwa kuripoti shule, huku wazazi wakitakiwa kuwapeleka shule na wakikaidi agizo hilo watachukuliwa hatua za kisheria
Na Sebastian Mnakaya
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha amewataka Wazazi na walezi mkoani humo kuwapeleka watoto wao shule wale waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na wasipofanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria.
Macha ameyasema leo katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa sekondari Bumva iliyopo katika kijiji cha Bumva halmashauri ya Msalala wilayani Kahama yenye dhamani ya zaidi ya shilingi milioni 600, ambapo amezitaka kila shule kubandika orodha za majina ya wanafunzi waliofaulu.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamring Macha katika akiwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga (Sebastian Mnakaya)
Aidha Macha ameitaka halmashauri hiyo kuwa na mpango wa kujenga mabweni na nyumba za walimu katika shule hiyo ili kuwa na mazingira rafiki na bora kwa wanafunzi wanaotokea mbali, huku akiipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akisoma taarifa ya ujenzi wa shule hiyo mkuu wa shule ya Mwl Nyerere Kafumu Songora, amesema kukamilika kwa shule hiyo itasaidia kwa wanafunzi kutokutembea umbali mrefu, huku mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Rose Manumba amesema wataendelea kutekeleza miradi mbalimbali kwa wakati na yenye ubora.
Baadhi wa wakazi wa kijiji cha Bumva wakizungumza na Kahama fm kwa nyakati tofuti wameishukuru serikali kwa kujenga shule hiyo ambayo itawasaidia kupunguza gharama za usafiri kutokana na ukaribu wa shule hiyo pamoja na kuondokana na kukatisha masomo kwa wanafunzi.
INSERT……….WANANCHI MUMVA

Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hasani imeendela kutoa fedha katika miradi mbalimbali ya maendeleo kwa mkoa wa shinyanga akiwemo kwenye sekta ya elimu, kilimo, mifugo, maji, afya na miundombinu ya barabara.