Kahama FM

Miaka 30 ya TRA, wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiari bila shuruti

2 July 2026, 3:04 pm

Mkuu wa wilaya ya Kahama, Frank Nkinda akizungumza na wafanyabiashara wakati wa hafla ya miaka 30 ya TRA (Picha na Sebastian Mnakaya)

‘Wafanyabiashara na wajasiliamali lipeni kodi kwa hiari ili kuleta maendeleo ya nchi yetu”

Mkuu wa wilaya ya Kahama, Frank Nkinda ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa kikodi Kahama kwa uendelea kushirikiana vyema na wafanyabiasha na wajasiliamali hali inayosababisha kulipa kodi kwa hiali bila ya shuruti.

Nkinda ametoa kauli hiyo katika hafla ya miaka 30 TRA pamoja na kuwashukuru walipakodi, ambapo amesema kuwa wafanyabiashara na wajasiliamali wamekuwa wakishirikiana vyema hasa katika ulipaji wa kodi kwa hiari bila kufukuzana kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma na sasa.

Aidha, ameipongeza TRA Kahama kwa kujenga urafiki na wafanyabiashara ili walipe kodi kwa wakati, pamoja na kushirikiana na kutatua changamoto wanazokutana nazo wafanyabiashara kwa mazungumzo.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda

Kaimu msaidizi wa meneja wa mkoa wa kikodi wilaya ya Kahama upande wa ukaguzi na ufatiliaji Esther Maliya, amesema kuwa Mamlaka imeendelea kuwa karibu na walipa kodi na kuweza kukaa meza moja na kutatua changomoto zinazowakabili huku wakiendelea kutoa elimu mara kwa mara.

Sauti ya Kaimu msaidizi wa meneja wa mkoa wa kikodi wilaya ya Kahama upande wa ukaguzi na ufatiliaji Esther Maliya

Kwa upande wake, mwenyekiti wa wafanyabiashara wilaya ya Kahama Charles Machali, amesema kuwa wafanyabaishara wamekuwa wakilipa kodi kwa hiari na kwa wakati pamoja na malalamiko kupungua ikilinganishwa ilivyokuwa kipindi cha awali.

Sauti ya mwenyekiti wa wafanyabiashara wilaya ya Kahama Charles Machali

Nao, baadhi wafanyabiashara wa wilaya ya Kahama, akiwemo Gradiwes Kisusi na Godfrey Chua, wameipongeza TRA kwa kurahisisha mifumo ya ulipaji kodi pamoja kusikiliza changamoto zao, huku awakisema kuwa zamani walikuwa wanawaogopa maafisa TRA ikilinganiswa sasa hali imekuwa tofauti.

Sauti za wafabiashara Kahama Gradiwes Kisusi na Godfrey Chua