Kahama FM

NGO’s Kahama zatakiwa kufanya kazi kwa uwazi

24 July 2026, 2:40 pm

Rehema Edison Msajili Msaidizi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga (Picha na Sebastian Mnakaya)

”Iwe mnafanya shughuli zenu kwa ufadhili ama kujitolea mnapaswa kuwa wazi na kutoa taariifa kwa serikali na hiyo ni kwa mujibu wa sheria”

Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayofanya kazi katika Wilaya ya Kahama yamehimizwa kutekeleza shughuli zake kwa uwazi na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za Serikali ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima.

Wito huo umetolewa na Rehema Edison Msajili Msaidizi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakati wa mkutano wa Jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Wilaya ya Kahama uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mchungaji Mwema.

Aidha, Rehema amesema ni muhimu mashirika yote kuweka wazi shughuli na miradi inayotekeleza pamoja na vyanzo vya rasilimali zake, hatua ambayo itasaidia kujenga uaminifu, kuimarisha ushirikiano na Serikali pamoja na kuongeza uwajibikaji kwa wananchi wanaonufaika na miradi hiyo.

Sauti ya Rehema Edison Msajili Msaidizi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Afisa tarafa wa tarafa ya Isagehe Asha

Kwa upande wake Afisa tarafa wa tarafa ya Isagehe Asha Makwita akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Kahama, Frank Nkinda amesema kuwa serikali imekuwa ikitambua michango mbalimbali ya kimaendeleo yanayotolewa na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Sauti ya Afisa tarafa wa tarafa ya Isagehe Asha

Jukwaa hilo limewakutanisha wadau mbalimbali wa mashirika yasiyo ya kiserikali kwa lengo la kujadili mbinu za kuimarisha uendelevu wa mashirika hayo kupitia ubunifu, ushirikiano wa kimkakati na matumizi ya vyanzo vya ndani vya rasilimali fedha.