Kahama FM

Vijana wa Nyahanga jitokezeni kuonyesha vipaji vyenu vya soka, kuelekea michuano ya Ngayiwa Jimbo Cup

30 August 2026, 3:22 pm

Diwani wa kata ya Nyahanga Josephina Kilimba akikagua timu katika ufunguzi wa michuano ya kutafuta wachezaji watakao iwakilisha katika michuano ya Ngayiwa Jimbo Cup (Picha na Sebastian Mnakaya)

‘‘Vijana ni wakati wenu sasa wa kuonyesha vipaji vyenu vya soka ili muweze kupata fursa mbalimbali za mchezo wa mpira wa miguu’’

Vijana wa kata ya Nyahanga Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuonyesha vipaji vyao vya kucheza mpira wa miguu katika kuelekea michuano ya Ngayiwa Jimbo Cup inayotarajiwa kuanza hivi karibuni, itakayo shirikisha kata 20.

Kata ya Nyahanga imeendelea na maandalizi ya kutafuta wachezaji watakayo iwakisha kata hiyo, kwa kucheza ligi ya timu tano kutoka katika mitaa mitatu, ambayo ni Nyahanga, Shunu na Mtakuja, ikiwa leo ni ufunguzi wa mashindano hayo na yameanza na timu ya Talent Boys na Hongwa Warriors. zilizoopo katika mtaa wa Nyahanga na Shunu.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Nyahanga, diwani wa kata ya Nyahanga Josephina Kilimba amewataka vijana hao kuongeza bidii katika kucheza mpira ili waweze kupata nafasi ya kucheza kwenye michuano ya Ngayiwa Jimbo Cup yanayoandaliwa na mbunge wa jimbo la Kahama mjini Benjamini Ngayiwa.

Sauti ya diwani wa kata ya Nyahanga Josephina Kilimba

Kwa upande wake, mwenyekiti wa mtaa wa Nyahanga Benard Mapalala amesema kuwa vijana wachangamkie fursa ya kuonyesha vipaji vyao kwa ajili kufika mbali katika mchezo wa mpira wa miguu.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa Nyahanga Benard Mapalala

Nae, Mratibu wa michuano hiyo ya Ngayiwa Jimbo Cup kata ya Nyahanga Gabriel Mvanga, amesema kuwa lengo la michuano hiyo ni kwa ajili ya kuunganisha vijana kwa pamoja na kuchagua vijana wenye vipaji ambao watakwenda kuiwakilisha timu ya kata ya Nyahanga katika michuano hiyo.

Sauti ya Mratibu wa michuano hiyo ya Ngayiwa Jimbo Cup kata ya Nyahanga Gabriel Mvanga

Hata hivyo, timu zitakazoshiriki katika kutafuta wachezaji wazuri watakayoiwakilisha timu ya Nyahanga ni pamoja na Talent Boys, Hongwa Worriores, Nyahanga Academy, Lugela na Young City.