Kahama FM
Kahama FM
8 September 2026, 11:26 pm

‘‘Kiongozi wa dini, Nabii Nicolaus Suguye, ametoa msaada wa matofali elfu tatu na mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa kituo cha kulelea watoto yatima, huku akitoa wito kwa jamii kujitokeza na kuwasaidia watoto hao’’
Kiongozi wa dini, Nabii Nicolaus Suguye, ametoa msaada wa matofali 3,000 na mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu Kahama Orphanage Center kilichoopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga ili kuboresha usalama wa watoto hao.

Msaada huo umeenda sambamba na mahitaji mbalimbali ya chakula na usafi, yakiwemo unga, mchele, mafuta ya kupikia, sabuni na maharage, kwa ajili ya watoto wanaoishi katika kituo hicho.Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo leo, kabla ya kuanza mkutano wa Injili katika Manispaa ya Kahama, Nabii Suguye amewataka wadau mbalimbali pamoja na watu wenye uwezo kuwa na moyo wa kuwasaidia watoto hao kwa kutoa misaada kulingana na nafasi na uwezo walio nao.
Katika hatua nyingine, akiwa katika kituo cha New Hope amesema kuwa pamoja na kutoa misaada, ni muhimu kwa jamii kuwa karibu na watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto yatima na kushirikiana katika kuhakikisha wanapata mahitaji muhimu.

Awali, msimamizi wa kituo cha Peace Orphanage Center Abubakari Issa amesema kituo hicho kina changamoto kubwa ya kukosa uzio unaofanya watoto au kudhurika na kuumwa na ubwa pamoja kuibiwa vitu mbalimbali katika kituo hicho.

Nao, baadhi ya watoto wanaishi katika vitu hivyo, akiwemo Judith Lucas na Seleman Josephat wa kituo cha New Hope wamemshukuru Nabii Suguye kwa kugushwa kwake kwa kuwapatia msaada huo, huku msimamizi wa kituo hicho Scolastika Fred akimuomba kuendele kuwa na moyo huo wa kutoa na kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Hata hivyo, Nabii Suguye ametembelea vituo viwili vya kulele watoto yatima na wanaishi katika mazingira magumu cha New Hope na Kahama Orphanage Center vilivyoopo katika kata ya Zongemela Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga kwa lengo la kutoa msaada vitu mbalimbali.
