Kahama FM

Makarani Kahama, wafundwa kuelekea Uchaguzi mdogo kata ya Zongomela

28 May 2026, 1:42 pm

Makarani waongozaji wa uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Zongomela wametakiwa kusoma Katiba sheria na miongozo ya tume ya uchaguzi Pamoja na kujiepusha kuwa vyanzo vya malalamiko kutoka katika vyama vya siasa.

Wito huo umetolewa na msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Kahama mjini Steven Magala wakati wa ufunguzi wa mafunzo Makarani waongozaji wa uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Zongomela.

Sauti ya msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Kahama mjini Steven Magala

Katika hatua nyingine Magala ametoa wito kwa makarani hao kuwahi katika vituo vya kupigia kura ikiwa ni Pamoja na kutoa kipaumbele kwa makundi maalumu.

Sauti ya msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Kahama mjini Steven Magala

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema kuwa watayatumia vyema mafunzo waliyoyapata kufanikisha uchaguzi huo na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kikatiba.

Sauti za makarani wilayani Kahama

Uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya  Zongomela unafanyika June Mosi mwaka huu kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo ambaye ni Meya mstaafu wa manispaa ya Kahama Ramdhani Bundala maarufu kwa jina la Ng’wana Ibengwe.