Kahama FM
Kahama FM
10 August 2026, 2:27 pm

Waziri wa Nishati Deogratius Ndejembi ambaye pia ni mlezi wa Kiserikali wa mkoa wa Shinyanga, amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya Kahama-Kakola kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 73.1 kwa gharama ya shilingi Bilioni 100.6 kuongeza kasi ya ujenzi ili kufungua fursa za kiuchumi katika mikoa ya Shinyanga na Geita.
Ndejembi ametoa agizo hilo leo baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo inayounganisha maeneo ya Kahama Mjini na Msalala, akisema Serikali haina mashaka na ubora wa kazi inayofanywa na mkandarasi, bali kinachohitajika ni kuongeza kasi ya utekelezaji.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROAD) mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Ntuli Mwaikokesya amesema kuwa hatua za ujenzi zinaendelea huku ifikapa desemba mkwa huu mradi huo utakuwa umekamilika.

Naye mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita amesema kuwa mradi huo ni wa kimkakati na utaweza kuboresha shughuli za kiuchumi, huku Mbunge wa Jimbo la Msalala Mabula Magangila akiomba kuwekwa taa kwenye barabara hiyo.
Hata hivyo, barabara ya Kahama–Kakola haionekani tena kama njia ya usafiri pekee, bali imeanza kutazamwa kama mhimili wa uchumi wa Kahama na Msalala.
