Kahama FM

DC Nkinda: TAKUKURU chunguza vikundi vya ukusanyaji ushuru soko la CDT

28 April 2026, 4:29 pm

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Frank Nkinda ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilayani humo kufanya uchunguzi kufuatia malalamiko ya baadhi ya wafanyabiashara kutozwa ushuru mkubwa pamoja na uwepo wa makusanyo yasiyo rasmi yanayowaumiza wafanyabiashara wadogo.

Na Mwandishi wetu

Nkinda ametoa agizo hilo akiwa katika soko la Namanga alipokutana na wafanyabiashara wa soko hilo kwa ajili ya kusikiliza kero zao na kuzitatua ambapo baadhi ya wafanyabiashara Irene Thomas na Michael Juma wamelalamikia kuwepo kwa kikundi miongozi mwao ambacho kimekuwa kikikusanya ushuru kutoka kwako kinyume na sharia.

Mmoja wa wafanyabiashara wa samamki Adam Jackson ambako ndicho kikundi kinacholalamikiwa akatolea ufafanuzi huku mwenyekiti wa soko hilo Juma Jumeji akieleza namna walivyoingia makubaliano ya kikundi hicho kukusanya mapato.

Sauti za wafanyabiashara wa soko la Namanga CDT

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Frank nkinda akaitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kahama kufuatilia na kuja na jibu sahihi ili limsaidie kutoa maamzisahihi.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Frank Nkinda