Kahama FM
Kahama FM
28 April 2026, 4:00 pm

Wakaguzi wakuu migodi mkoani Shinyanga wametakiwa kutoa taaifa za kweli na sahihi kwa kile kitakacho tokea katika migodi ili kuondoka na taarifa zinazoleta tahuruki kwa Jamii, pamoja na kuzingatia maadili ya uchimbaji.
Sebastian Mnakaya
Wito huo umetolewa leo na mwenyekiti wa Chama Cha Wachimbaji Wadogo Mkoa wa Shinyanga (SHIREMA) Hamza Tandiko, wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa mameneja na wakaguzi wakuu wa migodi ya wachimbaji wadogo kutoka Kahama, Mbongwe na Shinyanga.
Aidha, Tandiko amessisitiza umuhimu wa weredi kwa wachimbaji na utoaji wa taarifa sahihi za shughuli za uchimbaji, huku akipongeza wa wakaguzi katika kupunguza ajali na madhara migodini.

Kwa upande wake, katibu wa Chama cha Wakaguzi Kanda ya Kahama madini Idd Chacha, amesema kuwa usalama mgodi ni suala muhimu hasa katika kipindi cha mvua nyingi, huku akisisitiza taarifa sahihi wakati wa uchimbaji ili kuondokana na majanga mbalimbali yanayoteka katika migodi.

Nao, baadhi wa wachimbaji wa madini wilaya ya Kahama wakizungumza kwa nyakati tofauti, akiwemo Jackosin Mahona na Hassani Haruna wamesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuboresha katika shughuli zao cha uchimbaji hasa kupunguza ajali pamoja na kuwa na uelewa wa kutosha.
