Kahama FM
Kahama FM
17 August 2026, 12:27 pm

‘‘Vikundi rejesheni fedha mlizo kopa ili na vikundi vingine vipatiwe fedha hizo’’
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga imevipeleka vikindi 12 kwa kutofuata utaratibu wa kurejesha mikopo inayotolewa kwa fedha za mapato ya ndani ya 10% kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Hoja hiyo imeibuliwa leo kwenye kikao cha baraza la madiwani cha robo ya nne ya mwaka 2025/2026 Manispaa ya Kahama, na diwani wa kata ya Nyahanga Josephina Kilimba, amehoji hatima ya vikundi vilivyofikiswa Mahakamani wakitaka kujua hatua iliyofikia.

Aidha, Kilimba amesema vikundi hivyo vimeshindwa kurejesha fedha ipasavyo na mpaka sasa ni shilingi ngapi zimeweza kurejesha kwenye halmashauri baada ya kufikishwa mahakamani.

Afisa Maendeleo wa Manispaa ya Kahama Hamis Mnubi amesema kuwa sheria ya kuchukua mikopo halmashauri ni lazima ufuate utaratibu wa kulipa kidogo kidogo bila ya riba ili na wengine wakopeshwe lakini baadhi ya vikundi havijarejesha.
Vikundi hivyo ni Wapambanaji kutoka kata ya Nyahanga milioni 70.9, Jakasi kata ya Busoka million 24.5, Wajasiliamali kata ya Nyasubi million 27.9, Winner kata ya Kinaga milioni 10.5, huku vikundi vinne ambavyo wakopaji wake wakisambaratika na kupiga chenga ambo ni vikundi vya Lucha Future shilingi million 14.6, nguvu kazi milioni 11.6 na kikundi cha Umoja wa daladala milioni 7.16.
