Kahama FM
Kahama FM
16 June 2026, 12:25 am

‘‘Vijana wana uwezo mkubwa sana wa kulinda amani ya nchi yetu na kuwa na mshikamano wa pamoja wa kitaifa’’
Vijana wa kata ya Mhungula, katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kulinda uhuru, umoja na mshikamao wa ili kuendelea kuilinda amani na utulivu uliopo sasa nchini.
Kauli hiyo imetolewa na mkufunzi wa mafunzo ya itikadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kahama ambaye pia ni diwani wa kata ya Nyahamga Josephina Kilimba, wakati wa kikao cha mafunzo ya itikadi aliyofanyika katika kata ya Mhungula yakishirikisha makundi mbalimbali.

Aidha, Kilimba amewataka vijana wote kulinda amani ya nchi kwa gharama kubwa na kuwa na mshikamo thabiti ili nchi yetu iendelee kuwa kisima cha amani duniani na kujikita zaidi katika shughuli za kiuchumi.

Kwa upande wao baadhi ya vijana wa kata hiyo, akiwemo Hamidu Mrisho amesema kupitia mafunzo hayo imewasaidia kwa kiasi kikubwa kulinda amani na kuwa wamoja, huku Mariam Nyutoni akisema kuwa mafunzo hayo yanatija kwa vijana ili kujikwamu kiuchumi pamoja na kuipambania na kuilinda amani.
Hata hivyo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kahama kimetoa mafunzo kwa wanachama wake kwa makundi mbalimbali ili kukuwambusha na kufahamu umuhimu wa kuifuata itikadi ya chama hicho.