Kahama FM

Wakazi kata ya Kahama Mji wahitaji shule ya sekondari

13 May 2026, 2:07 pm

Diwani wa kata ya Kahama mjini Godson Andre akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani Manispaa ya Kahama (Sebastian Mnakaya)

”Wananchi wa kata ya Kahama mjini wanahitaji shule ya sekondari ili watoto wao waondokane na changamoto ya kusoma katika shule za kata jirani”

Wananchi wa kata ya Kahama mjini wilayani Kahama mkoani Shinyanga, wameiomba serikali kujengewa shule ya sekondari ili kuondokana na wanafunzi kusoma kata jirani.

Kauli hiyo imetolewa na diwani wa kata ya Kahama mjini Godson Andrew, wakati wa kikao cha baraza la madiwani la Manispaa ya Kahama cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2025/2026, ambacho kimepokea taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kila kata.

Aidha, Andrew amesema kuwa kata hiyo ambayo iko katikati mwa Manispaa ya Kahama haina shule ya sekondari hali inayowalazimsha wanafunzi kusoma kata za jirani ambapoa meiomba halmashauri kujenga shule kwenye kata hiyo.

Sauti ya diwani wa kata ya Kahama mjini Godson Andrew

Akijibu hoja hiyo,mkuu wa divisheni ya Mipango na uratibu wa Manispaa ya Kahama, Flora Sangiwa amekiri kuwepo na changamoto hiyo na kusema kuwa mipango inaendelea kutafuta eneo kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya gorofa kutokanana uhaba wa ardhi unaochangiwa na uwepo wa vitega uchumi vya wafanyabiashara.

Sauti ya mkuu wa divisheni ya Mipango na uratibu wa Manispaa ya Kahama Flora Sangiwa