Kahama FM
Kahama FM
15 May 2026, 5:14 pm

”Madiwani waomba barabara zikarabatiwa kutokana na kuharibiwa na mvua”
Wakala wa barabara Vijijini na Mjini (TARURA) wilayani Kahama mkoani Shinyanga, wametakiwa kuendelea kuzifanyia matengenezo barabara zilizoharibika kwa mvua ili wananchi waendelee na shughulu za kijamii na kiuchumi.
Hayo yamesemwa na diwani wa kata ya Idahina Mathias Makashi, katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya ushetu, ambapo amesema kuwa kata yake miundombinu ya barabara sio nzuri na kuomba serikali kuzikarabiti ili gari zipitike katika kipindim hiki cha mavuno.
Aidha, Makashi amesema kuwa kuna barabara ambazo zipo kwenye bajeti na nyingine hazipo na kuomba zitengewe bajeti, huku akisisitiza kuwa kuna baadhi ya barabara hazifunguki hali inayosababisha wananchi wakati wa kuuza mazao yao bei ya chini kutokana na barabara kuwa mbovu.

Akijibu hoja hiyo, kaimu meneja wa TARURA wilaya ya Kahama Mhandisi Manyango Nchambi amekiri kuwa barabara hizo ni mbovu na zitafanyiwa matengenezo kutoka na fedha zitavyopatikana, huku akisisitiza kuwa tayari wana mpango wa kuzifanyia matengenezo.