Kahama FM
Kahama FM
13 July 2026, 5:40 pm

‘‘Kukamilika kwa Mpango Kabambe wa Kidijitali itasaidia kuondoa makazi holela katka Manispaa ya Kahama’’
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga imetakiwa kuendelea kutoa ushirikiano katika kutekeleza mradi wa Mpango Kabambe wa Kidigitali na msimamizi wa mradi, unaotarajiwa kutekelezwa katika kata 20 za manispaa hiyo.
Kauli hiyo limetolewa na Afisa Mipango Miji Mkuu, kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayesimamia mradi ya TACTIC, Alex Mwamaso katika kikao cha kamati ya mradi wa Mpango Kabambe wa Kidijitali Manispaa ya Kahama.

Mwamaso, amewataka viongozi mbalimbali wa Manispaa hiyo na msimamizi wa mradi huo kushirikiana kikamilifu ili kumaliza kwa wakati utekelezaji wa mradi huo pamoja na kuendelea kuwaelimisha wananchi kuuelewa mpango huo.
Aidha, Mwamaso amesema kuwa kati ya miji 18 nchini, Manispaa ya Kahama pekee imefanikiwa kuwa ya mfano katika utekelezaji wa mradi wa Mpango Kabambe wa kidijitali unaotekelezwa huku miji mingine kuja kujifunza Kahama.

Kwa upande wake, meneja mradi wa Mpango Kabambe wa Kidijitali kutoke Urban Solution ltd William Kitonka, amesema kuwa wako tayari kushirikiana katika kutekeleza mradi huo, huku akiwaomba watumishi kuendelea kujifunza ili watakapo wakabidhi mradi huo watekeleze kusahihi kama ilivyokusudiwa.

Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halamshauri ya Mnaspaa ya Kahama, steven Magala amesema kuwa waendelea kutoa ushirikiano kwa msimazi wa mradi Urban Solution Ltd, huku akiwataka wanapokutana na changamoto wasisite kuziwakilisha kwako.