Kahama FM
Kahama FM
7 May 2026, 5:07 pm

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga limeombwa kupeleka nishati ya umeme katika shule ya Msingi Mlimani na Mtakuja ambazo tayari zimefungwa miundombinu ya umeme zilizoopo katika kata ya Nyahanga.
Akizungumza katika baraza la madiwani la Manispaa ya Kahama katika kikoa cha kawaida, diwani wa kata ya Nyahanga Josephina Kilimba akiuliza swali katika kikao hicho kuwa ni lini shule hizo zitapelekewa nishati ya umeme ili kuweza kurahishisha kazi katika shule hizo.
Aidha, Kilimba amesema kuwa kuna baadhi ya taasisi zikiwemo shule, zahanati na vituo vya afya katika maeneo mengine hazijafikiwa kupata nishati hiyo na kuomba serikali kushughulikia changamoto hiyo.

Kwa upande wake, Mhandisi kutoka TANESCO wilaya ya Kahama Ones Mbembe akijibu swali hilo amesema kuwa ndani ya mwaka wa fedha ujao katika maeneo ya taasisi ambayo hayajafikiwa na umeme yatafikiwa, huku kwa sasa wakifanyia kazi na watendaji wa kata katika kuainisha maeneo hayo.
Nae, mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kahama Thomas Myonga, mewapongeza na kuwataka madiwani wa Mnispaa ya Kahama kuendelea kuwatumikia wananchi kwa kusikiliza na kutatua kero zao.