Kahama FM
Kahama FM
15 August 2026, 8:24 pm

‘‘Katekelezeni ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2025/2030’’
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kahama mkoani Shinyanga wanayoisimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM 2025/20230, wametakuwa kuweka mifumo mizuri ya ufatiliaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili iweze kukamilika kwa wakati.
Kauli hiyo limetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda wakati wa kikao cha kupokea na kupitisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi mkuu wa 2025 kwa kipindi cha januari hadi juni 2025.
Aidha, Nkinda amesema kuwa wataaluma wanapaswa kutekeleza Ilani ya Ccm kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali pamoja na kuikamilisha kwa wakati katika sekta ya maji, umeme, elimu, afya na Miundombinu ya barabara.

Kwa upande wake, Katibu wa CCM wilaya ya Kahama Andrew Chitwanga, ameasema kuwa wenyeviti vijiji na vitongoji wanapaswa kufanya mikutano ya mara kwa mara wananchi kujua mapato na matumizi, huku wakihamasisha masuala ya maendeleo.

Baadhi ya wananchama wa CCM, akiwemo Molla za Zabroni na James Onyanga wameishukuru serikali kwa kuipatia fedha bilioni 295 wilaya ya Kahama kwa ajili ya kutekeleza miradi ya mbalimbali ya maendeleo, huku wakimuomba mkuu wa wilaya Nkinda kuifatilia ili ikamilike kwa wakati.
Ikumbukwe kuwa, wilaya ya Kahama ilipokea jumla shilingi bilioni 295.2 kwa ajili ya utekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa sasa.