Kahama FM

Wazazi Watakiwa Kuwekeza Zaidi Katika Elimu ya Watoto

26 September 2026, 12:52 am

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama Glory Absalum akizungumza katika mahafali ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Rwepa’s (Picha na Sebastian Mnakaya)

‘‘Malezi bora pamoja na elimu ni msingi muhimu wa kuwaandaa watoto kwa maisha yao ya baadaye’’

Wazazi wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuwekeza zaidi katika elimu ya watoto wao, na kuwa elimu ni urithi muhimu unaoweza kuwasaidia watoto katika maisha yao popote watakapokwenda.

Wito huo umetolewa leo na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama Glory Absalum, wakati wa mahafali ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Rwepa’s, ambapo amesema wazazi hawapaswi kujikita katika kuwaachia watoto mali pekee kama vile mashamba na magari, bali wanapaswa kuhakikisha wanawapatia elimu itakayowawezesha kujitegemea na kujitafutia maisha yao.

Aidha, amewataka wazazi kuhakikisha wanawalinda watoto wanaomaliza kidato cha nne kwa kuwaweka chini ya uangalizi wao wakati wakisubiri matokeo, badala ya kuwaacha kwenda kuishi kwa ndugu.

Sauti ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama Glory Absalum
Mkurugenzi wa shule ya sekondari Rwepa’s Frank Samweli akizungumza na wanafunzi na wazazi wa shule hiyo

Nae, mkurugenzi wa shule ya sekondari Rwepa’s Frank Samweli, amesekuwa wanaishuruku serikali kwa kuwapa fursa ya kutoa huduma ya elimu pamoja na kuwasaidia watoto kwa kujiandaa kupata taaluma mbalimbali, huku akisisitiza kuwa watoto wanaosoma katika shule hiyo wako salama.

Sauti ya mkurugenzi wa shule ya sekondari Rwepa’s Frank Samweli

Kwa upande wao, baadhi ya wazazi akiwemo Samola Salaganda na Juna Chiza wamesema sekta binafsi imekuwa kifanya vizuri katika sekta ya elimu na kuomba serikali kuzisaidia katika kuboresha mazingira pamoja na kutoa ushirikiano utakaosaidia wanafunzi kuendelea kufanya vizuri zaidi.

Sauti za wazazi Samola Salaganda na Juna Chiza

Awali, wahitumi wa kidato shule katika shule hiyo akisoma risala Lavishe Derick amesema kuwa shule hiyo ina maabara ya kisasa na maktaba, huku ikikabiliana na changamoto kwa baadhi ya wazazi kutokulipa ada kwa wakati pamoja na kutohudhuria vikao vya shule, na kuwaomba wazazi kuondokana na changamoto hizo ili wanafunzi wasome bila kusumbuliwa.

Sauti ya msoma risala Lavishe Derick