Kahama FM

Viongozi Kahama watakiwa kusimamia mapato, migogoro ya ardhi

6 October 2026, 12:43 pm

Mkuu wa wilaya ya Kahama Dkt Francis Mlacha akikabidhiwa ofisi baada ya aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo kuhamishiwa wilaya ya Mkalama (Picha na Sebastian Mnakaya)

”Tunahitaji kuongeza mapato na kushughulikia changamoto mbalimbali zinazo wakabili wananchi wa wilaya ya Kahama”

Viongozi mbalimbali wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo, kuongeza na kudhibiti mapato, pamoja na kushughulikia migogoro ya ardhi na changamoto ya barabara.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Dkt. Francis Mlacha, wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika katika Manispaa ya Kahama, baada ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Frank Nkinda, kuhamishiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama.

Dkt. Mlacha amesema atashirikiana na viongozi wa wilaya hiyo katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi, pamoja na kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Dkt. Francis Mlacha

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Frank Nkinda, amemtaka Dkt. Mlacha kujiandaa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Kahama, ikiwemo migogoro ya ardhi na ubovu wa barabara.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Frank Nkinda

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kahama, Thomas Muyonga, amesema changamoto kubwa zinazoikabili wilaya hiyo ni barabara na migogoro ya ardhi, huku kusimamia ipasavyo miradi ya maendeleo na kushirikiana na halmashauri tatu zilizopo katika wilaya hiyo.

Sauti ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kahama, Thomas Muyonga