Kahama FM

Mwabomba waiomba serikali kuharakisha ujenzi wa kituo cha polisi

15 October 2026, 11:45 am

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magom akizungumza na wananchi wa kata ya Idahina iliyopo halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani shinyanga (Picha na Sebastian Mnakaya)

Wananchi wa Mwabomba wataka ujenzi wa kituo cha polisi upewe kipaumbele kuimarisha usalama.

Wananchi wa Kijiji cha Mwabomba, Kata ya Idahina, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga wameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa kituo cha polisi ili kuimarisha usalama katika eneo hilo.

Akizungumza wakati wa ziara ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi, mwananchi Sospeter Bulendi amesema matukio ya ujambazi yamepungua kutokana na ushirikiano kati ya wananchi na Jeshi la Polisi.

Sauti ya mwananchi Sospeter Bulendi

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Idahina, Mathias Makashi, amesema kituo hicho kitasaidia wananchi kuendelea na shughuli zao za kiuchumi bila hofu ya uhalifu.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Idahina, Mathias Makashi

Naye, Kamanda Magomi amewataka wananchi kuichukulia Polisi kama rafiki na kutoa taarifa za uhalifu, akieleza kuwa ekari mbili tayari zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha polisi katika kata hiyo.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magom

Amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya wananchi na Jeshi la Polisi ni muhimu katika kuimarisha ulinzi na usalama wa jamii.