Kahama FM

Hali ya Usalama Barabarani Shinyanga Yatajwa Kuwa Shwari

29 September 2026, 10:11 pm

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi akizungumza na madereva katika sendi kuu ya mabasi wilaya ya Kahama (Picha na Sebastian Mnakaya)

‘‘Madereva shinyanga watakiwa kuzingatia sheria ili kuepuka hatua za kisheria’’

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limewahakikishia Madereva na watumiaji wote wa barabara, wakiwemo wasafiri wa mabasi na malori, kuwa usalama wao unaendelea kuimarishwa na kuwataka kuendelea na ratiba zao za usafiri kama kawaida.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi ameyasema hayo baada ya kutokea kwa mgomo wa madereva na kudai kuwa hali ya usalama katika barabara pamoja na maeneo mengine ya mkoa huo ni salama.

Aidha, Kamanda magomi amewataka madereva wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani pamoja na kuepuka makosa ambayo yanaweza kuwafanya wachukuliwe hatua za kisheria.

Sauti ya Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi