Kahama FM

Wananchi Kahama Watakiwa Kutumia E-Ardhi Kupata Hatimiliki kwa Urahisi

29 September 2026, 2:50 pm

Zoezi la kliniki ya ardhi linaloendelea katika Ofisi za Kata ya Mwendakulima (Picha na Sebastian Mnakaya)

”Wananchi Kahama Wahamasishwa Kutumia E-Ardhi Kupata Huduma za Ardhi Bila Kufika Ofisini”

Wananchi wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kutumia mfumo wa kidijitali (E-Ardhi) ili kupata huduma mbalimbali za ardhi kwa urahisi ikiwemo kupata hatimiliki bila kulazimika kufika katika ofisi za ardhi.

Akizungumza katika zoezi la kliniki ya ardhi linaloendelea katika Ofisi za Kata ya Mwendakulima afisa ardhi mteule kutoka Manispaa ya Kahama Richard Mayiku, amesema Serikali imeanzisha mfumo huo kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma za ardhi kwa kuwawezesha wananchi kupata huduma kwa njia ya kidijitali.

Mayiku amesema kupitia mfumo wa e-ardhi wananchi wanaweza kupata huduma bila kufika moja kwa moja katika ofisi za ardhi jambo ambalo linaongeza ufanisi na kupunguza muda wa wananchi kufuatilia huduma hizo.

Sauti ya afisa ardhi mteule kutoka Manispaa ya Kahama Richard Mayiku

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliopata huduma kupitia mfumo huo wameipongeza serikali kwa hatua, na wakieleza kuwa unarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi

Sauti za baadhi ya wananchi

Hata hivyo, wananchi ambao hawafahamu namna ya kutumia mfumo huo ofisi ya ardhi Kahama imeandaa dawati maalumu kwa ajili ya kuwaelekeza na kuwasaidia namna ya kutumia mfumo pamoja na huduma nyingine zinazopatikana kwa njia ya mtandao.