Kahama FM
Kahama FM
6 November 2026, 1:05 pm

Wataalamu wa ardhi watakiwa kusimamia maeneo ya umma kuepuka migogoro
Wananchi wa Kata ya Mhongolo katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa ardhi na kuepuka kujenga katika maeneo yasiyoruhusiwa ili kuzuia migogoro ya matumizi ya ardhi wakati wa utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Kahama ya Kidijitali.
Wito huo umetolewa na diwani wa Kata ya Mhongolo, Mariamu Galula Sasi, wakati wa mkutano wa kujadili Mpango Kabambe wa matumizi ya ardhi, ambapo amewashukuru wataalamu kwa kuwapatia elimu kuhusu mipango bora ya ujenzi na matumizi ya ardhi.

Amesema ni muhimu wananchi kupata maelekezo kutoka kitengo cha ardhi cha Halmashauri kabla ya kuanza ujenzi ili kuepuka kuwekeza katika maeneo yaliyotengwa na Serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Aidha, ameiomba Halmashauri kuhakikisha maeneo yaliyotengwa kwa matumizi mbalimbali ya umma yanasimamiwa kwa uaminifu na weledi, akieleza kuwa usimamizi usiozingatia utaratibu unaweza kusababisha wananchi kujenga nyumba na kufanya uwekezaji mkubwa katika maeneo ambayo baadaye wanaweza kuondolewa, hali inayoweza kuibua migogoro.

Nao, baadhi wa wananchi wa kata hiyo, akiwemeo Marry Lymo na Jacksoni Msele wameomba idara ya ardhi Manispaa ya Kahama kuendelea kuto elimu juu ya umhuhimu wa jenga nyumba ukiwa na kibadi cha ujenzi utakaosaidia kuondokana na ujenzi holela.

Afisa Habari na Mawasiliano wa Mradi wa Mpango Kabambe wa Kidijitali, Hamisi Mkoma amesema kuwa kwa sasa wananchi hawapaswi ufanya ujenzi bila ya kuwa na vibali vya ujenzi, huku wakitakiwa kutouzina maeneo kiholela ili kuondokana na migogoro ya ardhi.
Mpango Kabambe wa Kahama ya Kidijitali unalenga kuweka utaratibu bora wa matumizi ya ardhi na kuelekeza ukuaji wa mji kwa kuzingatia mahitaji ya sasa na ya baadaye ya wananchi.