Kahama FM

Mradi wa barabara ya Kahama–Kakola wafikia asilimia 89.1

12 October 2026, 9:57 am

Ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami ya Kahama-Kakola ukiendelea (Picha na Sebastian)

Ujenzi wa barabara ya lami Kahama-Kakola unatarajiwa kukamilika desemba 7, 2026

Mradi wa ujenzi wa barabara ya Kahama–Kakola wenye urefu wa kilomita 73, unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 100.6 mkoani Shinyanga, unatarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi wa mkoa huo na mikoa jirani kwa kurahisisha shughuli za kiuchumi zikiwemo madini, kilimo na mifugo.

Akizungumza kuhusu maendeleo ya mradi huo, Msimamizi wa Mradi kutoka kitengo cha kihandisi na Ushauri TECU, Marco Bee, amesema hayo na kwamba ujenzi wa barabara hiyo utarahisisha usafiri na Kuondoa changamoto zilizokuwa zikiwakabili watumiaji., ikiwemo matope wakati wa mvua na vumbi wakati wa kiangazi.

Sauti ya msimamizi wa mradi kutoka kampuni ya TECU, Mhandisi Marco Bee

Kwa upande wake, Mhandisi Samsoni Mgila, anayesimamia uzalishaji wa kokoto, zege na lami zinazotumika katika ujenzi wa barabara hiyo ya kiwango cha lami, ameeleza hatua mbalimbali zinazozingatiwa kuhakikisha vifaa vinavyozalishwa vinafikia viwango vinavyohitajika kwa ajili ya ujenzi huo.

Sauti ya Mhandisi Samsoni Mgila

Nao, baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Shinyanga, akiwemo CPA Elibariki Mangowi na Noela Mapolu, wamewashukuru viongozi wa wakala hao kwa kuwapatia fursa ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na kusimamiwa na taasisi hiyo.

Wamesema ziara hiyo imewasaidia kufahamu kwa vitendo namna shughuli zinazopangwa na ofisi zinavyotekelezwa katika maeneo ya miradi, pamoja na kujionea utekelezaji wake na namna unavyolingana na malengo yaliyokusudiwa.

Sauti ya wafanyakazi wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga CPA Elibariki Mangowi na Noela Mapolu