Kahama FM

Wananchi mwanase waomba kujengwa shule mpya ya sekondari

1 October 2026, 1:58 pm

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala, Judica Sumari akizungumza na wananchi wa kata ya Mwanase wakatika wa mkutano wa hadhara wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga (Picha na Sebastian Mnakaya)

‘‘Halmashauri ya Msalala kujenga shule nne za sekondari kwa kata zilizo na wanafunzi wengi’’

Na mwandishi wetu

WANANCHI wa Kata ya Mwanase, katika Halmashauri ya Msalala, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, wameiomba Serikali kujenga shule nyingine ya sekondari katika kata hiyo, ili kuwaondolea wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu kufuata elimu.

Wananchi hao wametoa ombi hilo katika mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, wakati akisikiliza kero na changamoto zinazowakabili wananchi wa Kata ya Mwanase.

Wamesema ukosefu wa shule ya kutosha katika eneo hilo umekuwa ukilazimu baadhi ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda shuleni, hali wanayodai inaweza kuwaathiri katika masomo yao.

Sauti za wananchi wa kata ya Mwanase

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala, Judica Sumari, amesema Kata ya Mwanase ni miongoni mwa maeneo yatakayofaidika na mpango wa Serikali wa ujenzi wa shule mpya za sekondari katika awamu inayofuata.

Sauti ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala, Judica Sumari

Naye Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mabula Magangila, amesema Halmashauri hiyo imepanga kujenga shule mpya za sekondari katika kata nne, hatua inayolenga kupunguza umbali ambao wanafunzi hutembea kwenda shuleni.

Sauti ya mbunge wa jimbo la Msalala

Mbunge huyo pia ametangaza kuchangia kiasi cha shilingi milioni 10 kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa shule katika kata ya hiyo ya mwanase.