Kahama FM

TAKUKURU yadhibiti upotevu wa mapato, yarejesha mil. 236 Shinyanga

16 November 2026, 1:19 pm

Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Mwamba Masanja akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Shinyanga (Picha na Sebastian Mnakaya)

Milioni 236 zarejeshwa kupitia operesheni za TAKUKURU shinyanga.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga imefanikiwa kurejesha jumla ya Shilingi 236,069,957.63 katika kipindi cha Aprili hadi Septemba 2026, kupitia udhibiti wa makusanyo ya mapato ya ndani, ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma, uchunguzi na mashtaka.

Akizungumza kuhusu mafanikio hayo, Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Mwamba Masanja, amesema fedha hizo zimepatikana kupitia hatua mbalimbali zilizochukuliwa na taasisi hiyo katika maeneo tofauti ya mkoa huo.

Sauti ya Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Mwamba Masanja

Katika hatua nyingine, taasisi hiyo imefanikisha ukusanyaji wa Shilingi 35,129,844.63 kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kutoka kwa wadaiwa sugu wa ushuru wa huduma (Service Levy) waliokuwa wamekwepa kulipa kwa muda mrefu.

Sauti ya Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Mwamba Masanja

Masanja amesema ufuatiliaji huo ulibaini kutowasilishwa kwa baadhi ya malipo ya kodi ya zuio (Withholding Tax), ambapo baada ya uchunguzi wa kina kiasi cha Shilingi 2,692,139 kililipwa.

Sauti ya Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Mwamba Masanja