Kahama FM

Zaidi ya wananchi 51,000 kunufaika na ujenzi wa wodi ya wazazi Kakola

23 August 2026, 5:14 pm

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Wazo Mwang’onda ameweka jiwe la msingi kwenye jengo la wodi ya wazazi kwenye kituo cha Afya Kakola (Sebastian Mnakaya)

“Serikali kuu ilileta shilingi Milioni 250  na Halmashauri ya Msasa imetoa  zaidi ya shilingi Milioni 19  kwa kuboresha miundombinu   ya kituo hicho’’

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Wazo Mwang’onda ameweka jiwe la msingi kwenye jengo la wodi ya wazazi kwenye kituo cha Afya Kakola kata ya Bulyanhulu  Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kilichogharimu zaidi ya shilingi Milioni 269.

Mganga mfawidhi wa kituo hicho Dkt Emanuel Boniface akisoma taarifa ya ujenzi huo

Kabla ya kuweka jiwe hilo Mganga mfawidhi wa kituo hicho dkt  Emanuel Boniface akisoma taarifa ya ujenzi huo leo  amesema  ujenzi ulianza rasmi mwezi Oktoba mwaka 2025 na kukamilika mwaka 2026 mwezi Julai.

Sauti ya Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Kakola Dkt Emanuel Boniface

Mbunge wa jimbo la Msalala  Mabula Magangila amesema kuwa kwa mujibu wa sensa  ya watu na makazi ya mwaka 2022 kata ya kakola ina takribani wakazi 51,000 lakini  walikuwa hawana kituo cha afya kulikuwa na Zahanati tu.

Sauti ya Mbunge wa jimbo la Msalala  Mabula Magangila

Mwang’onda amesema kuwa katika kata hiyo kulikuwa hakuna kituo afya hali iliyosababisha wananchi kwenda kutafuta huduma mbali, ila kwa sasa watapata huduma ya afya karibu, huku akipongeza halmashauri hiyo kusimamia vizuri wakandarasi kwani jengo hilo limejengwa kwa kiwango kizuri.

Sauti ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Wazo Mwang’onda