Kahama FM

Wananchi wa mtaa wa Mtakuja wamweleza Mbunge kilio chao cha maji

29 September 2026, 3:33 pm

Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, Benjamini Ngayiwa akikagua miundombinu ya maji katika mtaa wa Mtakuja kata ya Nyahanga Manispaa ya Shinyanga (Picha na Sebastian Mnakaya)

‘‘Wananchi wa mtaa wa Mtakuja waiomba Serikali kuwafikishia huduma ya maji licha ya kujitolea kuchimba mitaro’’

Wananchi wa Mtaa wa Mtakuja Kata ya Nyahanga Manispaa ya Kahama wameiomba Serikali kuwafikishia huduma ya maji, licha ya juhudi walizofanya kwa kujitolea kuchimba mitaro kwa ajili ya kupitisha mabomba ya maji bado huduma hiyo haijawafikia

Wananchi hao wametoa wamesema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo hilo na Mbunge wa Jimbo la Kahama mjini, Benjamini Ngaiwa wakati wa mkutano wa kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

Wananchi wamesema licha ya kushiriki katika zoezi la uchimbaji wa mitaro na hatua nyingine zilizochukuliwa kwa ajili ya kuhakikisha huduma ya maji inawafikia, bado wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji.

Sauti za wananchi wa mtaa wa mtakuja

Akitoa ufafanuzi kuhusu changamoto hiyo Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Kahama, KUWASA John Mkama, amesema eneo hilo lilikuwa likikabiliwa na changamoto ya kijiografia, hali iliyofanya upatikanaji wa maji ya kutosha kuwa mgumu bila kujengwa kwa tanki la maji.

Amesema kwa sasa ujenzi wa tanki hilo umekamilika, hivyo hatua inayofuata ni kuhakikisha huduma ya maji inasambazwa kwa wananchi wa eneo hilo.

Sauti ya Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Kahama, KUWASA John Mkama

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, Benjamini Ngayiwa, ameitaka Mamlaka ya Maji Kahama kuchukua hatua za haraka za kukamilisha usambazaji wa mabomba ili wananchi waweze kupata huduma ya maji.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Kahama mjini, Benjamini Ngaiwa

Awali, Diwani wa Kata ya Nyahanga, Josephine Kirimba amesema ni kweli wananchi walishiriki katika zoezi la kuchimba mitaro kwa ajili ya kupitisha mabomba ya maji, huku mabomba hayo yakiwa yamefikishwa katika eneo hilo.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Nyahanga, Josephine Kirimba

Hata hivyo, wananchi bado wanasubiri huduma hiyo kuanza kutolewa kikamilifu baada ya kukamilika kwa miundombinu muhimu, ikiwemo tanki la maji.