Kahama FM

DC Nkinda atatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 5

9 September 2025, 3:04 pm

Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda na mwekezaji Tenth Maruhe (Picha na Sebastian Mnakaya)

”kwa mujibu wa sheria za ardhi, kutokana na maelezo ya afisa ardhi na mwekezaji mzawa Tenth Maruhe ametoa maagizo barabara hiyo kuondolewa ilipo kwa sasa na badala yake irudishwe kwenye mchoro wa ramani wa awali unavyoonyesha”

Na Sebastian Mnakaya

Idara ya Ardhi ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga imetakiwa kuondoa barabara iliyopita katika viwanja vya mwekezaji mzawa Tenth Maruhe katika kata ya Busoka ili aendelee na uwekezaji katika eneo hilo lilikuwa na mgogoro Kwa zaidi ya miaka 5.

Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda wakati wa ziara yake ya kutembelea eneo hilo na kusikiliza mgogoro huo, kwa pande zote mbili za mwekezaji huyo na maafisa wa idara ya ardhi katika Manispaa hiyo.

Aidha Nkinda amesema kwa mujibu wa sheria za ardhi, kutokana na maelezo ya afisa ardhi na mwekezaji mzawa Tenth Maruhe ametoa maagizo barabara hiyo kuondolewa ilipo kwa sasa na badala yake irudishwe kwenye mchoro wa ramani wa awali unavyoonyesha.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda

Awali mmiliki wa eneo hilo la Busoka Tenth Maruhe akitoa malalamika yake mbele ya mkuu wa wilaya hiyo, amesema mgogoro huo ni wamuda mrefu wa barabara kuingia kwenye eneo lake, huku akiomba kutatuliwa changamoto hiyo ili aanze kuliendeleza eneo hilo kwa uwekezaji.

Sauti ya mmiliki wa eneo hilo Tenth Maruhe
Maafisa ardhi wa Manispaa ya Kahama

Afisa Ardhi wa Manispaa ya Kahama Lameck Evalist amesema baada ya ramani kukosea katika eneo hilo walibadilisha na kupitisha barabara katika eneo hilo, huku wakiwashirikisha na wananchi wa eneo hilo kufanya uamuzi huo.

Sauti ya Afisa Ardhi wa Manispaa ya Kahama Lameck Evalist

Hata hivyo afisa ardhi mteule wa Manispaa ya Kahama Mashili Magesa amesema mwekezaji huyo alinunua eneo hilo baada ya kuvutiwa kwa kuwepo na bava zone, huku baada ya miaka kaadha ramani ya mchoro wa eneo hilo lilikosewa na kufanyiwa marekebisho hali iliyosababisha kutokea kwa mgogoro huo.